MUUNDO WA DCU

DCU ni taasisi ya kiserikali iliopo , chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati. Taasisi hii imeundwa na Mamlaka zote kumi na moja za Serikali za Mitaa ziliopo Zanzibar ambazo ni Manispaa ya Mjini, Magharibi A, Magharibi B, Baraza la Mji wa Chake Chake, Wete, Mkoani, Halmashauri ya Kusini, Kati, Kaskazini A, Kaskazini B, na Michweni pamoja na baadhi ya Taasisi za Serikali Kuu zinazohusiana na ujenzi ambazo ni Idara ya Mipango Miji, Mamlaka ya Kuendeleza na Kusimamia Mji Mkongowe, Wakala wa Majengo na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar pia ni sehemu ya DCU ikiwakilisha sekta binafsi.

Muundo wa DCU


Hadi, mwaka wa 2020, DCU iliundwa na Kamati ya wajumbe kumi na saba (17) na kamati mbili za kitaalamu ambazo ni:

  • Idara ya Mipango Miji na Vijiji (Mwenyekiti)
  • Mamlaka ya Kuendeleza na Kuhifadhi Mji Mkongwe
  • Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Zanzibar (ZEMA)
  • Wakala wa Majengo Zanzibar
  • Bodi ya Wasanifu, Wahandisi wa Wataalam Zanzibar
  • Manispaa ya Mji wa Zanzibar
  • Baraza la Manispaa ya Wilaya yala Magharibi A
  • Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharibi B
  • Baraza la Mji wa Chake-Chake
  • Baraza la Mji wa Wete
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kusini
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini A
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B
  • Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni
  • Baraza la Mji wa Mkoani
  • Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima

  • DHAMIRA YA DCU



    Ni Kuongeza udhibiti wa maendeleo kupitia ufanisi, mfumo wa uwazi na shirikishi wa matumizi endelevu ya ardhi na maendeleo hapa Zanzibar

    Copyright ©2024 DCU