Matangazo / Taarifa
DCu inatoa kibali cha kukamilika kwa jengo kabla ya kuanza kutumia jengo hilo.
DCU imedhamiria Kufikia 2020, vibali vyote vya maendeleo ya ardhi Zanzibar viwe vimetolewa.
KAMATI YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA UJENZI

Kamati ya Usimamizi na Udhibiti Ujenzi (Development Control Unit (DCU) imeundwa kwa mujibu wa Kifungu Cha tano (5) cha Kanuni ya Udhibiti wa Ujenzi ya mwaka 2015. Kanuni hiyo imetayarishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 12 & 37cha Sheria ya Mipango Miji na Vijiji sura ya 85 ya mwaka 1955 (Town and Country Planning Decree of 1955). Sheria hiyo ndio pekee kwa Zanzibar yenye kipengele kinachohusu usimamizi na udhibiti ujenzi. DCU ilianza kufanya kazi zake rasmi mwaka 2015 kufuatia kutolewa Tangazo Rasmi la Kisheria Nambari 38 la mwaka 2015 (L.N 38/2015).DCU inafanya kazi zake kwa kuunganisha nguvu baina ya Mamlaka zote kumi na moja za Serikali za Mitaa ziliopo Zanzibar ambazo ni Manispaa ya Mjini, Magharibi A, Magharibi B, Baraza la Mji wa Chake Chake, Wete, Mkoani, Halmashauri ya Kusini, Kati, Kaskazini A, Kaskazini B, na Michweni pamoja na baadhi ya Taasisi za Serikali Kuu zinazohusiana na ujenzi ambazo ni Idara ya Mipango Miji, Mamlaka ya Kuendeleza na Kusimamia Mji Mkongowe, Wakala wa Majengo na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA). Aidha, Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar pia ni sehemu ya DCU ikiwakilisha sekta binafsi.

soma zaidi

Dhamira ya DCU

Kuongeza udhibiti wa maendeleo kupitia ufanisi, mfumo wa uwazi na shirikishi wa matumizi endelevu ya ardhi Zanzibar

DCU pia inasimamia uhifadhi wa maeneo ya kihistoria. pichani ni STONE TOWN

Habari Mpya na Matukio

New zanzibar map

Maeneo zilipo ofisi za DCU Unguja na Pemba

Copyright ©2024 DCU