KAMATI YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA UJENZI

Kamati ya Usimamizi na Udhibiti Ujenzi (Development Control Unit (DCU) imeundwa kwa mujibu wa Kifungu Cha tano (5) cha Kanuni ya Udhibiti wa Ujenzi ya mwaka 2015. Kanuni hiyo imetayarishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 12 & 37cha Sheria ya Mipango Miji na Vijiji sura ya 85 ya mwaka 1955 (Town and Country Planning Decree of 1955). Sheria hiyo ndio pekee kwa Zanzibar yenye kipengele kinachohusu usimamizi na udhibiti ujenzi. DCU ilianza kufanya kazi zake rasmi mwaka 2015 kufuatia kutolewa Tangazo Rasmi la Kisheria Nambari 38 la mwaka 2015 (L.N 38/2015).DCU inafanya kazi zake kwa kuunganisha nguvu baina ya Mamlaka zote kumi na moja za Serikali za Mitaa ziliopo Zanzibar ambazo ni Manispaa ya Mjini, Magharibi A, Magharibi B, Baraza la Mji wa Chake Chake, Wete, Mkoani, Halmashauri ya Kusini, Kati, Kaskazini A, Kaskazini B, na Michweni pamoja na baadhi ya Taasisi za Serikali Kuu zinazohusiana na ujenzi ambazo ni Idara ya Mipango Miji, Mamlaka ya Kuendeleza na Kusimamia Mji Mkongowe, Wakala wa Majengo na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA). Aidha, Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar pia ni sehemu ya DCU ikiwakilisha sekta binafsi.

Lengo kuu la kuanzishwa kwa DCU ni kusimamia kazi za utoaji wa vibali vya ujenzi na kudhibiti ujenzi holela na usiofuata taratibu. Kuanzishwa kwa DCU, kumesaidia sana kuondoa tatizo lilokuwepo la kutokua na chombo madhubuti cha usimamizi na udhibiti ujenzi kinachotambulika kisheria.


DHAMIRA YA DCU



Ni Kuongeza udhibiti wa maendeleo kupitia ufanisi, mfumo wa uwazi na shirikishi wa matumizi endelevu ya ardhi na maendeleo hapa Zanzibar

Copyright ©2024 DCU